Tuesday, August 23, 2011

BAADHI YA WABUNGE WAPINGA KUUNGA MKONO BAJETI YA WIZARA YA MAJI!

Baadhi ya wabunge wamekataa kuunga mkono hoja ya wizara ya maji, na kuitaka Serikali kuchukua hatua juu tatizo la miradi ya maji nchini hasa ule wa Benki ya dunia, pamoja na kutimiza ahadi za kutekeleza miradi hiyo vijijini kwa kuwa ndilo eneo linalotaabika kwa kiasi kikubwa kwa sasa.

Akichangia hoja ya wizara hiyo bungeni leo mjini Dodoma, Mh. Mbunge Nimrod Elirehema Mkono(CCM) anayeiwakilisha Musoma Vijijini, amebainisha kuwepo kwa mtandao mkubwa unaoanzia serikalini, wizarani, mpaka katika halmashauri ya Musoma, unaozipeleka fedha za miradi ya maji Musoma mjini na kuitelekeza Musoma vijijini, na kwamba ataushikilia msimammo wake wa kutounga hoja mkono mpaka kieleweke.


Nae Mbunge wa Mchinga(CCM) Said Mohamed Mtanda, amesema hayuko tayari kuona na kuvumilia watendaji wanaoiangusha serikali.

No comments:

Post a Comment