Wednesday, July 6, 2011

HUU NI WARAKA KUTOKA KWA MGANGA MACHINU MWANANDALA KUTOKA SHINYANGA!

Mganga maarufu kutoka kijiji cha mwakata mkoa wa shinyanga bwana MACHINU MWANANDALA ameishauri serikali kuwafatilia kwa karibu waganga wa jadi wanaofanya kazi hiyo kwa kutumia matangazo barabarani kama wanaouwezo wa kurefusha na kunenepesha viunga vya binaadam.

Amesema kwa sasa imejengeka tabia ya matangazo ya aina hiyo ambayo kwa mtazamo wake anayaona matangazo hayo kuwa na dalili za kitapeli kwa waganga wa aina hiyo ambao wengi wao wanaweka matangazo hayo katika miji mikubwa.

Akitoa ushahidi juu ya tiba zake anazozitoa bwana MWANANDALA amesema yeye ametoa tiba za asili kwa zaidi ya miaka ishirini sasa kwa kutumia mitishamba ndani na nje ya nchi lakini haelewi dawa yeyote ambayo inaweza kunenepesha makalio au kiungo chochote cha binaadam.


Mganga huyo ambae kwa sasa anao jumla ya watoto arubaini na tisa na jumla ya wake wanne ndie mganga maarufu kabisa katika kijiji hicho ambapo watu kutoka sehemu mbali mbali wanamiminika katika boma lake kupata tiba za asili.

No comments:

Post a Comment