Tuesday, August 23, 2011

BENKI KUU YASEMA UWEPO WA NOTI BANDIA UNACHAGIWA NA KUKUA KWA TEKNOLOJIA!

SERIKALI imesema kuwepo kwa matumizi ya noti bandia zilizo katika mzunguko, kunachangiwa na maendeleo ya kasi ya vifaa vya elektroniki, vyenye uwezo mkubwa wa kunakili picha za rangi .

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa fedha, PEREIRA AME SILIMA, katika kipindi cha maswali na majibu kwa niaba ya waziri wa fedha Mh. Mustapha Mkulo, ambapo amesema sakata la noti bandia kwa kiasi kikubwa limezikumba nchi nyingi duniani, na kwamba si kosa la wafanyakazi wa benki kuu kama linavyofikiriwa na wananchi walio wengi.


Aidha waziri huyo amewaondoa shaka watanzania juu ya ubora wa noti mpya, na kuwataka kuamini kwamba noti mpya zina ubora na serikali iko makini dhidi ya watu wanaoghushi noti hizo.

No comments:

Post a Comment