Wednesday, March 21, 2012

BIDHAA SOKO LA TEMEKE STEREO ZAPANDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 100 HADI 200!

Uharibifu wa miundombinu hususani katika maeneo ya vijijini ni changamoto kubwa inayowakabili wakulima wakati wanapotaka kusafirisha mazao yao kuyapeleka sokoni hali inayoathiri upatikanaji wa vyakula kwenye masoko mbalimbali nchini.



Hali hiyo ndio iliyolikumba soko la Temeke Stereo Jijini Dar es Salaam ambako kutokana na uharibifu huo wa miundombinu, uliofuatiwa na kipindi cha ukame na mvua bei ya bidhaa sokoni hapo imepanda kwa zaidi ya asilimia 100 hadi 200 na kusababisha mfumuko wa bei ya vyakula.


Afisa Masoko Manispaa ya Temeke Bw TITO NOMBO amesema hali hiyo pia imesababisha baadhi ya bidhaa ikiwemo viazi vitamu kutoka Tanzania bara kuadimika na wafanyabiashara kuamua kuingiza viazi hivyo kutokea Zanzibar.
                                                                  Picha kwa Hisani ya wadau!

No comments:

Post a Comment