Monday, October 17, 2011

WANAFUNZI 172 SHULE YA MSINGI PERA BAGAMOYO WATUMIA MADAWATI 8 KUKALIA!

Wanafunzi 172 katika Shule ya Msingi Pera iliyopo kata ya Kibindu ,Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani wanalazimika kutumia madawati Nane kati ya Kumi yaliyopo ambapo mawili yanatumika katika ofisi ya walimu kutokana na kukabiliwa na ukosefu wa madawati shuleni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari shuleni hapo baada ya Mbunge wa jimbo la Chalinze SAID BWANAMDOGO kutembelea shule hiyo ,Mkuu wa shule ya Msingi Pera Mwl RAMADHANI MGONGO amesema japo wanakabiliana na hali hiyo lakini bado inaleta madhara ya wanafunzi kukohoa mara kwa mara.


Mwl MGONGO amebainisha kuwa mazingira ya wanafunzi kusoma na kufundishwa hayaridhishi kwa kiasi kikubwa pamoja na maisha ya walimu kwani hadi sasa hawana nyumba za kuishi hivyo wanaishi katika nyumba walizozijenga kwa nguvu zao ambazo wamezijenga kwa tope na kuezeka nyasi.


Aidha vitabu wanavyotumia kufundishia na vifaa haviendani na mitaala iliyopo na havina hadhi kwani ni miaka mitatu hawajapelekewa suala linalosababisha kufundishia vitabu vilivyochakaa huku vikiwa havina baadhi ya kurasa.


Mwl MGONGO amesema kwa upande wake anawaunga mkono walimu wanaokimbia na kukataa kwenda kufundisha shule zilizo katika mazingira yasiyoridhisha kuishi kwani ni vigumu kukubali kuishi katika nyumba ya tope.

No comments:

Post a Comment