Thursday, June 30, 2011

TAMISEMI YAOMBWA KUONGEZA KIPINDI CHA MUDA WA MAFUNZO KWA MADIWANI!

Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI imeombwa kuongeza kipindi cha muda wa mafunzo kwa madiwani kutoka cha wiki moja kilichotangazwa na serikali ili watendaji hao kufanya kazi yao ipasavyo.


CONCHESTA RWAMLAZA Mbunge wa Viti Maalum Chadema amesema ili madiwani waweze kukabiliana na Wakurugenzi wa Manispaa wababe serikali inatakiwa kuwapa mafunzo endelevu na sio semina semina za wiki moja ambazo haziwaondolei uoga wa kutetea fedha za miradi.

Kwa upande wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera ameomba serikali iongeze madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali hususani waliobobea kwenye magonjwa ya wanawake ili waungane na wawili wanaotoa huduma kwa sasa.

No comments:

Post a Comment