Monday, May 16, 2011

SIKU YA UWASHWAJI MISHUMAA KUWAKUMBUKA WALIOKUFA KWA UKIMWI ILIVYOADHIMISHWA NA KLABU YA SAVE LIFE!

                                       Hii ndio mishumaa iliyowashwa wakati maadhimisho hayo
                     Wanachama na wadau wa Klabu ya Save Life wakiwa kwenye picha ya pamoja
                               Muda wa kuwasha mishumaa uliwadia, kila mtu akiwa tayari kwa tukio
 Washiriki wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa Ukimwi

Klabu ya Save Life ya Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba cha Muhimbili (MUHAS) imeadhimisha siku ya uwashwaji mishumaa kukumbuka watu waliokufa kwa ugonjwa wa ukimwi kwa kuendesha mdahalo uliwashirikisha wadau mbalimbali wanaopiga vita kuenea kwa VVU.



Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Klabu Save life CELESTINE MPIZI amesema lengo la maadhimisho hayo sio kuwasha mishumaa peke yake ila pia kuibua hisia za jamii ifahamu kwamba ugonjwa wa ukimwi upo na unaendelea kuua maelfu ya watu duniani.


Wakichangia mada baadhi wa washiriki wa mdahalo huo wamesema kuishi na virusi vya Ukimwi nchini ni changamoto inayowakabili waathirika walioamua kujitangaza kutokana na vitendo vya unyanyapaa vinavyowakabili.


Kauli Mbiu ya maadhimisho Siku ya uwashwaji mishumaa kwa mwaka huu ilikuwa ni ‘Gusa Maisha’.

1 comment:

  1. Hongereni sana wana muhas mkiongozwa na mwenyekiti wenu na classmet wangu CELESTINE MPILI kwa kufanya tukio muhimu na la heshima ya pekee linalopaswa kuigwa na jamii yote hususan sisi tulio katika hii kada ya afya. narudia tena kwa kusema hongereni sana. its FRANK M KABISSI wa kcmc.

    ReplyDelete