Afisa Tarafa Bw. Peter Masidi akifungua rasmi vyumba viwili vya madarasa ya shule ya Sekondari Lusaka yaliyojengwa kwa msaada wa Vodacom Foundation yenye thamani ya shilingi milioni 37 (kulia) ni Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule.
Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule akimshukuru Afisa Elimu ya Sekondari Wilayaya Sumbawanga Bi. Emilia Fungo mara baada ya hafla fupi ya kukabidhi vyumba viwili vya madarasa ya Shule ya sekondari Lusaka wilayani humo vyenye thamani ya sh. Milioni 37 viivyojengwa kwa msaada wa Vodacom Foundation.
Kikundi cha wanawake kikitoa burudani katika hafla fupi ya makabidhiano ya madarasa mawili yaliyojengwa kwa msaada wa Vodacom Foundation kwa Shule ya Sekondari Lusaka Wilayaya Sumbawanga.
No comments:
Post a Comment