Saturday, February 4, 2012

MAFUNDI WACHAKARIKA KUSHONA SARE 400 ZA VIJANA WA GWARIDE MAALUM KITAFA LA MIAKA 35 YA CCM

 MAFUNDI 20 waliopewa kazi wa kushona sare zitakazovalishwa na Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wakati wa gwaride maalum siku ya kilele ya miaka 35 ya CCM wakiwa kazini jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambako sherehe za maadhimimisho hayo kitaifa zitafanyika Jumapili hii. Jumla ya vijana 400 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza watashiriki gwaride hilo.

 Uwanja wa CCM Kirumba zitakakofanyika kitaifa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM, Jumapili hii, Februari 5, 2012, ukiwa umepambwa maneno ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Chama, Rais Jakaya Kikwete ambaye atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment