Tuesday, December 6, 2011

JESHI LA POLISI NA SUMATRA LAWATAKA WAMILIKI KUTOPANDISHA NAULI ZA MIKOANI!

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi kavu (Sumatra), limewataka wamiliki na mawakala wa mabasi yaendayo mikoani na nchi za jirani kuacha kujipangia nauli bila kuzingatia sheria ya nauli elekezi iliyotolewa na mamlaka hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda MOHAMED MPINGA amewataka mawakala wa mabasi kutimiza wajibu wao na kuzingatia sheria ambazo zimewekwa hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.


Mmoja ya mawakala hao ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Morimori Bw KIDAKULI NGONYANI amewalalamikia baadhi ya wamiliki kushindwa kutekeleza sheria zilizopo na ameiomba SUMATRA kuitisha kikao na wamiliki ili waeleze mapungufu yanayojitokeza.


Hata hivyo Mkurugenzi Mkaguzi wa Kanuni za Barabarani SUMATRA, Mhandisi ARON KISAKA amepokea malalamiko hayo na kuahidi kuyafanyia kazi.

No comments:

Post a Comment