Tuesday, November 15, 2011

DALADALA ZAGOMA KIGOGO KUISHINIKIZA SERIKALI KUKARABATI ENEO KOROFI LA KIGOGO RANDA BAR!

Baadhi ya wakazi wa Kigogo jijini Dar es Salaam na wale wanaotumia usafiri wa daladala kutoka katikati ya jiji wamekumbana na adha ya usafiri baada ya mabasi yanayotoa huduma kwenye barabara hiyo kugoma ili kuishinikiza serikali ikarabati eneo korofi ambalo limekuwa likiharibu magari yao.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya madreva wa daladala yanayotoa huduma kwenye barabara hiyo wamesema licha ya kuiomba serikali kufukia mashimo kwenye eneo la Kigogo Randa Bar, suala lao halifanyiwa kazi jambo linalochangia magari yao kuharibika.


Kwa mwaka 2011 mgomo huu ni wa pili ukifuatiwa na wa kwanza uliofanyika Aprili ambapo Mkandarasi wa Manispaa ya Kinondoni alifika katika eneo hilo na kuweka kifusi ambacho kimeondolewa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam wakiwa kituoni eneo la Kigogo Mwisho kusubiri usafiri kuelekea katikati ya jiji kufuatia mgomo huo.

No comments:

Post a Comment