Saturday, October 1, 2011

VODACOM FOUNDATION YACHANGIA MADAWATI YA 45 MILIONI SHULE ZA MSINGI TEMEKE!

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana (kulia)akimpa mkono wa shukurani Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule mara baada ya kukabidhiwa madawati 250 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 22 kwa ajili ya shule za msingi tano za Wilaya ya Temeke,Shule zilizofaidika na msaada huo ni Mgulani, Tandika, Kizuiani, Muongozo, Kilamba, Hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Mgulani jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana (kulia)akisalimiana na moja ya wanafunzi wa shule ya Msingi Mgulani ambapo alifika shuleni hapo kupokea msaada wa madawati 250 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 22 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya shule za msingi tano za Wilaya ya Temeke,Shule zilizofaidika na msaada huo ni Mgulani, Tandika, Kizuiani, Muongozo, Kilamba, Hafla hiyo imefanyika katika shule ya msingi Mgulani jijini Dares Salaam. Anaeshuhudia kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana akiwasalimu baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Mgulani mara alipofika shuleni hapo kupokea msaada wa madawati 250 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 22 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya shule za msingi tano za Wilaya ya Temeke,Shule zilizofaidika na msaada huo ni Mgulani, Tandika, Kizuiani, Muongozo, anaeangalia kushoto Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule, Hafla hiyo imefanyika katika shule ya Msingi Mgulani jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Mgulani wakifurahia jambo wakati wa makabidhiano rasmi ya msaada wa madawati 250 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 22 kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya shule za msingi tano za Wilaya ya Temeke,Shule zilizofaidika na msaada huo ni Mgulani, Tandika, Kizuiani, Muongozo.
Kama ilivyo kawaida Kiduku kilikuwa ndio mtindo wa kuwaaga wageni waliokuja na msaada huo....Maaama leeeeeee Sindilela Maaaama leeeeeh Sindela, Duh palikuwa hapatoshi hapa.
* Ni awamu ya pili kampeni ya madawati 1000. Lengo kupunguza uhaba wa madawati S/msingi

Ikiendelza utamaduni wake wa kusaidia jamii kwa lengo la kubadili maisha mfuko wa kusaidia jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom leo umekabidhi madawati mia mbili na hamsini ikiwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya kampeni ya utoaji wa madawati katika shule za msingi katika mkoa wa Dar es salaam yanayofikia madawati mia tano yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni arobaini na tano.


Akikabidhi madawati hayo leo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambae anakaimu pia Ukuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Jordan Rugimbana, Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule amesema kampuni yake inatambua umuhimu wa elimu kwa watoto wa kitanzania kama amana muhimu ya kuwajengea mazingira ya maisha bora ya kujitegemea na pia kulisadia taifa.


"Inaumiza sana unapoona watoto wameketi sakafuni au kubanana katika dawati moja darasani, hii lazima itapunguza uwezo wao wa uelewa na ufuatiliaji masomo da ndio maana Vodacom kampuni inayoungwa mkono na watanzania zaidi ya milioni kumi ikaamua kuonesha upendo kwa kuwa na kampeni kamambe ya kusaidia madawati mashuleni"Amesema Mkuu wa Vodacom Foundation.


Jumla ya madawati 1000 yenye thamani ya shilingi 89,000,000/= yatakuwa yametolewa na Vodacom kwa shule za msingi kati ya April na Oktoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment