Mratibu wa Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI) unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD Bw. Ralf Ernst akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari yenye lengo la kujenga ufahamu miongoni mwao katika kuelekea kufanyika mkutano wa Maendeleo endelevu Rio+20 utakaofanyika kuanzia Juni 20-22 nchini Brazil kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kikundi cha Mazingira ambaye pia ndio Naibu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bi.Louise Chamberlain. Kulia ni Gertrude Lyatuu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "THE FUTURE WE WANT".
Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro akizungumza kuhusu umuhimu wa mkutano wa Rio+20 na maana yake katika kuipeleka dunia pale inapotaka kwenda. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi na kushoto ni Aifsa Mkuu wa Utafiti wa Masuala ya Mazingira katika Ofisi hiyo Dkt. Constantine Shayo
Afisa Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Stella Vuzo akimkaribisha Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akifafanua kuwa Tanzania kama mwanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabianchi amesema Tanzania imeandaa Rasimu ya Ripoti ya Rio+20 itakayojadiliwa na mkutano huo.
Bw. Muyungi alitumia fursa hiyo kuwakilisha mada kuhusiana na maendeleo endelevu ya Tanzania katika miaka 20 tangu mwaka wa kwanza kufanyika mkutano wa kwanza wa RIO iliyohusu "wapi tulipokuwa na wapi tulipo sasa".
Washiriki kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wakiwa katika warsha inayohusiana na mkutano wa Rio+20 iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa katika kusheherekea maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani
Washiriki kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wakiwa katika warsha inayohusiana na mkutano wa Rio+20 iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa katika kusheherekea maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani
No comments:
Post a Comment