Watanzania kote nchini wameshauriwa kuzidisha kiwango cha ufanyaji kazi katika maeneo yao ili kusaidia kuongezeka kwa pato la taifa katika kufikia kipindi cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Akizungumza kuhusiana na uzinduzi wa Promosheni ya wiki mbili ya maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwa kinywaji cha Konyagi kinachozalishwa na Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo DAVID MGWASSA amesema ufanyaji kazi kwa bidii ndiyo utakaowainua wateja wao kutoka kwenye umaskini.
Lengo la kuanzishwa kwa Kampuni ya Konyagi mwaka 1972 lilikuwa ni kupambana na unywaji wa pombe haramu ya gongo na kutengeneza kinywaji kilicho safi na salama kwa wanywaji.
No comments:
Post a Comment