Serikali inadaiwa jumla ya shilingi Bilioni 425 za ujenzi wa miradi ya Barabara hali iliyosababisha baadhi ya miradi kusimama, mingine kusuasua katika ujenzi na wakandarasi wengine kutoa notisi ya kusimamisha ujenzi huo.
Deni hilo limebainishwa na Kamati ya Bunge ya Miundombinu ambayo imesema kuchelewa kulipwa kwa deni hilo kunachelewesha maendeleo na kuongeza deni kutokana na mikataba ya ujenzi iliyosainiwa ambapo mkandarasi anapaswa kulipwa kama Serikali itashindwa kutoa fedha za utekelezaji wa mradi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo na mbunge wa Kigoma Mjini Bwana PETER SERUKAMBA amesema wanatarajia kukutana na Waziri Mkuu ili kuangalia uwezekano wa kulipa deni hilo hata kwa kukopa huku akitaja barabara ambazo ujenzi umesitishwa.
Aidha kamati hiyo ya Bunge ya miundombinu imeshauri Serikali na wadau wengine kukaa pamoja ili kuangalia upya sheria za ardhi kwa lengo la kuondoa kero ya bomoa bomoa ambayo imekuwa ikiwakumba wananchi mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment