KESI inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na mwenzake, imesikilizwa hii leo na watuhumiwa hao watatoa utetezi kwa siku tatu kuanzia Oktoba 18 hadi 20, mwaka huu.
Profesa Mahalu na aliyekuwa mshauri kwenye ubalozi huo, Grace Martin wanakabiliwa na mashitaka ya kuhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh bilioni mbili.
Profesa Mahalu na Bi Grace Martin, wanakabiliwa na mashitaka sita likiwemo la kuhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh. bilioni mbili kutokana na ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.
Wote kwa pamoja Wanadaiwa kutenda makosa hayo wakati wakiwa watumishi wa serikali. Kesi hiyo leo ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa, mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Mustapha Siyani. Hakimu Siyani amesema kesi hiyo itasikilizwa tena kuanzia Oktoba 18hadi 20, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment