Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha maombolezo cha Harith Mwapachu, ambaye ni mtoto wa Juma Mwapachu, aliyefariki dunia leo asubuhi.Kulia ni Balozi Juma Mwapachu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mke wa Balozi Juma Mwapachu, Rose Mwapachu, wakati alipofika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo jioni kumpa pole kufuatia kifo cha mtoto wake, Harith Mwapachu kilichotokea leo asubuhi, Oktoba 11, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Freeman Mbowe, wakati walipokutana katika msiba wa mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, Harith Mwapachu nyumbani kwa Mwapachu Mikocheni jijini Dar es Salaam leo Oktoba 11.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waombolezaji, wakati akiondoka nyumbani kwa Balozi Juma Mwapachu, wakati alipofika kutoa pole kufuatia kifo cha mtoto wa Balozi Juma Mwapachu, Harith Mwapachu leo Oktoba 11. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
No comments:
Post a Comment