Sunday, October 23, 2011

MH JOHN MNYIKA KUPELEKA BINAFSI MUSWADA WA SHERIA BUNGENI ILI KUDHIBITI BEI ZA BIDHAA NCHINI!

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Jijini Dar es salaam kupitia CHADEMA, JOHN MNYIKA anatarajia kupeleka Mswaada binafsi wa Sherika kwenye Vikao vya bunge lijalo Mjini Dodoma ili kudhibiti bei za bidhaa nchini ambazo zimetajwa kusababisha kupanda kwa gharama za maisha.

Akizunguza Jijini Dar es salaam, MNYIKA amesema amefikia uamuzi huo kutokana na hali hiyo iliyosababishwa pia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania kutishia uchumi wa wananchi pamoja na usalama wa taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment