Monday, October 31, 2011

MADIWANI SHINYANGA WAIKATAA TAARIFA YA FEDHA YA MAPATO!

Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wameikataa taarifa ya fedha ya mapato ya ndani kwa madai kuwa hayaendani na vyanzo vilivyopo ndani ya Manispaa hiyo.

Akizungumza na kituo hiki mmoja wa Madiwani hao, SEBASTIAN PETER, amesema kuwa taarifa hiyo imejaa urasimu hivyo hawawezi kuipokea kwa kujinufaisha wenyewe.


Kwa upande wa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bwana FESTO KANG’OMBE, ameunda kamati ya kuchunguza ikiwa ni pamoja na kuangalia upya idadi ya vyanzo vya mapato pamoja na vyumba vya kulala, vileo, majengo na masoko.

No comments:

Post a Comment