Wednesday, October 12, 2011

CCM YASIKITISHWA NA VITENDO VINAVYOFANYWA NA WAASI WA CHAMA HICHO IKIWEMO UCHOCHEZI!

Chama cha Mapinduzi CCM kimesikitishwa na baadhi ya vitendo vinavyofanywa na kikundi kidogo kilichopo ndani ya chama hicho za kupotosha na kushawishi kubadili maamuzi ya chama hicho.

Katibu wa Halamshauri kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCCM Bwana NAPE NNAUYE amesema kikundi hicho ambacho kina nguvu ya pesa ndani ya chama wanadaiwa kujaribu kuweka fitna katika uchaguzi uliofanyika IGUNGA ili CCM ishindwe kabisa kuchukua jimbo hilo ili waheshimiane

Wakati huo huo Bwana NAPE akizungumzia sakata la DOWANS amesema anashangazwa na hatua ya baadhi ya vyama vya siasa na wanaharakati nchini kutaka kufanya maandamano kwa ajili ya kuishiniza serikali kutoilipa DOWANS badala ya kutafuta namna ya kulitatua suala hilo kisheria zaidi.

No comments:

Post a Comment