Monday, October 31, 2011

MAHAKAMA YA ARDHI ILALA YAAMURU SERIKALI YA MTAA SHARIF SHAMBA KUBOMOA OFISI ZAKE KWENYE ENEO LA WAZI!

Mahakama ya Ardhi ya wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imeamuru kuvunjwa kwa jengo lililojengwa na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Ilala Sharif Shamba katika eneo la wazi lililopo kiwanja namba 227 karibu na Msikiti wa Ilala Sharif Shamba ambalo lilikuwa kero na kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo.

Wakizungumzia maamuzi ya kesi hiyo namba 210 ya mwaka 2011 baadhi ya wakazi hao ambao nyumba zao zilizingirwa na jengo hilo, wamewaomba watendaji wa serikali kuwa na kauli moja wanapotekeleza majukumu yao.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ilala Sharif Shamba Bw MTORO MAISHAA amesema kitendo kilichofanywa na mawakala wa mahakama kimekiuka sheria kwani kimefanyika bila ofisi yake kupewa taarifa yoyote.

No comments:

Post a Comment