Tuesday, September 27, 2011

SERIKALI YASEMA MALIPO YA WAATHIRIKA WA MABOMU GONGO LA MBOTO YANAFANYIKA KWA AWAMU!

Serikali imesema malalamiko yanayoendelea kujitokeza kuhusiana na malipo ya fidia kwa waathirika wa milipuko ya mabomu kwenye kambi ya Jeshi Gongolamboto yanatokana na ufafanuzi duni inayotolewa na Watendaji wa maeneo hayo kuhusu zoezi hilo.

Mratibu wa Maafa Wilaya ya Ilala jijini DSM, MWASABWITE ELLIOTH amesema mchakato wa malipo vifaa vya ndani kwa waathirika umetangazwa kuanzia kwenye kata ya Majohe na utaendelea kwenye maeneo mengine na kwamba kamati hiyo inaendelea kupokea malalamiko ya wananchi wasiofikiwa.


Kwa upande wake mmoja ya baadhi ya waathirika wa mabomu hayo Bwana MAULID MDEKA ameiomba serikali badala ya kuwalipa wahanga hao fedha wawalipe fidia ili kuondoa mgongano unaojitokeza.

No comments:

Post a Comment