Kituo cha sheria na haki za binadamu ambacho kinaratibu muungano wa asasi sizizo za kiserikali 16 ambao wamesajiliwa kuwa waangalizi wa ndani wa uchaguzi , wametoa taarifa yao ya awali kuhusu hali ya uchaguzi mdogo wa IGUNGA mkoani TABORA na kubaini mapungufu mbalimbali ikiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu.
Mwenyekiti wa muungano wa asasi hizo Bi MARTINA KABISAMA amesema pia kukosekana kwa maboresho ya daftari la kudumu la mpiga kura kwa sababu takwimu za wapiga kura waliojiandikisha katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 ndizo zitakazotumika katika uchaguzi mdogo IGUNGA.
Nae Kaimu mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi IMELDA URIO amelalamikia kitendo cha baadhi ya viongozi wa serikali kwenda huko IGUNGA na hivyo kushindwa kutenganisha majukumu ya kisiasa na yale yanayohusu utendaji wa jumla wa serikali.
Uchaguzi huo ambao unafanyika kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa na mbunge wa siku nyingi kwenye jimbo hilo ROSTAM AZIZ aliyejiuzulu nafasi hiyo unatarajiwa kufanyika Octoba 2 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment