Zikiwa zimebaki siku tano ili Kampeni za uchaguzi mdogo Ubunge jimbo la Igunga zikamilike, Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetangaza kutoridhishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na baadhi ya vyama vya siasa vinavyoshiriki kampeni hizo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Muda wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Prof AMON CHALIGHA amevitaja baadhi ya vitendo hivyo kuwa ni pamoja na ile yabaadhi viongozi kupanda jukwaani wakiwa na silaha, kurusha hewani risasi za moto na kutumia lugha za makabila badala ya lugha yak Kiswahili ambayo inakubalika.
Katika hatua nyingine Prof CHALIGA amebainisha kuwa wanashindwa kuzungumzia baadhi ya matukio ya uvunjifu huo wa amani kutokana na matukio hayo kufikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment