Ardhi Oevu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa ANNA TIBAIJUKA amesema Serikali inafanya utaratibu wa kuboresha fidia ya ardhi kwa wananchi ili iendane na bei ya soko kwa lengo la kuondoa malalamiko.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa watendaji wa wizara hiyo, maofisa ardhi kutoka Halmashauri zote nchini na sekta binafsi zilizowekeza katika ardhi, profesa TIBAIJUKA amesema katika maeneo yanayolalamikiwa kwenye wizara hiyo ni pamoja na suala la fidia huku akiwataka maofisa hao kuja na mkakati wa kuwawezesha wananchi kumiliki nyumba badala ya ardhi.
Aidha Waziri huyo ameendelea kusisitiza msimamo wake wa kufuta hati za maeneo ya wazi na kutoa notisi kwa wote waliojenga katika maeneo hayo ili wajitambue na kujua kwamba wanapaswa kuondoka kabla zoezi la bomoa bomoa halijawakuta.
Profesa ANNA TIBAIJUKA-Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
No comments:
Post a Comment