Monday, September 26, 2011

JAJI MKUU OTHMANI CHANDE AKIRI TANZANIA KUKABILIWA NA UHABA WA MAWAKILI WA KIJITEGEMEA!

Jaji Mkuu OTHMAN CHANDE amekiri kuwa Tanzania inakabiliwa na uhaba wa mawakili wa kujitegemea ukilinganisha na idadi ya wananachi ambao wanahitaji msaada wa kisheria ili waweze kudai au kutetea haki zao hasa waendapo mahakamani.

Akizungumza katika sherehe za kutimiza miaka 16 ya kituo cha sheria na haki za binadamu iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa jengo la Jaji MWALUSANYA lililoko KINONDONI jijini DSM , Jaji CHANDE amesema mpaka sasa kuna mawakili wa kujitegemea 2001 ambao ni wachache, hatua ambayo inawafanya baadhi ya wananchi kushindwa kusaidiwa kisheria mahakamani ambako wakati mwingine haki haipatikani.


Aidha Jaji Mkuu amesema kuna changamoto nyingi zinazozikumba baadhi ya mahakama nchini katika utoaji haki , kutokana na uwepo wa sheria za mila kandamizi ,hivyo wakati umefika kwa serikali kukamilisha sera ya Taifa ya msaada wa sheria ili badae Bunge litunge sheria itakayosimamia utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi walio na kipato cha chini.

No comments:

Post a Comment