Mgombea wa ubunge jimbo la Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. DALALY PETER KAFUMU amerejesha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi na kusema anao uhakika wa kutapata ushindi usio na shaka.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fomu hizo ili kuteuliwa rasmi kuwa mgombea, DK. KAFUMU pia ametaja mikakati yake kuwa ni pamoja na kuifanya Igunga kuwa ya kisasa kimaendeleo.
DK. KAFUMU amesema , miongoni mwa atakayoyapa kipaumbele katika kuijenga Igunga ni uboreshaji wa huduma za maji, uboreshaji miundombinu ya barabara hadi vijijini ikiwemo inayounganisha Igunga na Manonga.
Uchaguzi mdogo jimbo la Igunga umepangwa kufanyika Oktoba 2, mwaka huu kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo ROSTAM AZIZ kujiuzulu kutokana na sababu za kisiasa.
No comments:
Post a Comment