Kitendo cha serikali kutowaunganisha wasanii nchini kimechangia fani hiyo kuonekana kama isiyo na tija na inafanywa kama wito baada ya watu wanaojihusisha na kazi hiyo kutonufaika na matunda ya nguvu kazi yao.
Mhadhiri wa Sanaa Idara ya Sanaa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM CHARLES KAYOKA amesema kufikia miaka 50 tangu chuo hicho kianzishwe sekta ya sanaa imebaki kuwa kama mtoto yatima.
Kutokana na hilo Mhadhiri KAYOKA ameiomba serikali kuwawezesha wasanii wadogo wadogo kwa kuwapa mitaji ili waweze kuboresha kazi zao na hatimaye kujiletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment