Thursday, August 4, 2011

OFISI YA KATA KINONDONI YAPOKEA VIFAA VYA USAFI VYA MILIONI 1.3/-!

Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Kinondoni imepokea vifaa vya usafi vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.3 kutoka kwa kampuni ya Mawalla Holdings Limited ikiwa ni utekelezaji wa kusafisha mazingira katika kata ya Kinondoni,

Mkurugenzi wa kampuni ya Mawalla Holdings Limited, JOSEPH NUWAMANYA amewaomba watendaji wa Ofisi hiyo kuutumia mchango huo wa vifaa kutekeleza mkakati wa Manispaa ya Kinondoni katika kuweka mazingira safi.


Sambamba na hatua hiyo Diwani wa kata ya Kinondoni HUSNA HEMEDI amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza kutekeleza ilani yake kwa vitendo ikiwemo kutengeneza barabara za maeneo mbalimbali ili kurahisisha huduma za kijamii.

No comments:

Post a Comment