Thursday, August 4, 2011

SERIKALI YAKIRI UBIA KATI YAKE NA RITES HAUKUWA NA TIJA!

Serikali imekiri ubia kati yake na Kampuni ya Rites Consortium ya India uliounda Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) haukuwa na tija na kuamua kusitisha mkataba wake na kulirudisha chini ya uendeshaji wa serikali kwa asilimia mia.

Akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2011/2012, Waziri wa Uchukuzi OMARI NUNDU amesema hadi kufikia Julai 26, 2011 taratibu zote za kusitisha ubia zilikamilishwa na serikali inafanya taratibu za kulipatia bodi na menejimenti ya kudumu shirika hilo.


Wabunge wengi waliochangia bajeti hiyo akiwemo Mheshimiwa MARIA HEWA wamepinga kupitishwa kwa bajeti hiyo mpaka watakapohakikishiwa upatikanaji wa huduma za reli na ndege nchini.

No comments:

Post a Comment