Sunday, June 26, 2011

MAKAMU WA RAIS ALIVYOTEMBELEA FAMILIA YA MAREHEMU CHILUBA!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba, aliyefariki hivi karibuni. Makamu wa Rais alifika kuweka saini katika kitabu hicho kilichopo katika makazi ya Balozi wa Zambia nchini, jijini Dar es Salaam leo Juni 24. Picha na Amour Nassor-OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Zambia nchini baada ya kuwasili kwenye makazi ya Ubalozi huo leo Juzi 24 kwa ajili ya kuweka saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba. Kushoto ni Balozi wa Zambia nchini, Mavis Lengalenga Muyunda.

No comments:

Post a Comment