Mwigulu akimnadi mgombea ubunge wa CCM, Sioi Sumari katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana mji mdogo wa Mbuguni Kata ya Mbuguni, Arumeru Mshariki.
Mgombea wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akiomba kura mamia ya wananchi waliohudhutria mkutano wa kampeni za CCM katika mji mdogo wa Mbuguni, Kata ya Mbuguni.
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa mji mdogo wa Mbuguni Kata ya Mbuguni.
Vijana wakimshangilia Sioi kwenye mkutano wa mji mdogo wa Mbuguni.Malikia wa mipasho Khadija Omari Kopa na wasanii wenake wa kundi la Tanzania One Thetre (TOT) wakishambulia jukwaa kwenye mkutano wa mji mdogo wa Mbuguni, Arumeru Mashariki.
Mkurugenzi wa Tanzania One Thetre (TOT) kapteni John Komba ambaye pia ni Mjumbe wa Hlamashauri Kuu ya Taifa ya CCM, akiimba mbele ya umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni za CCM, mji mdogo wa Mbuguni jimbo la Arumeru Mashariki.
Mratibu wa Kampeni za CCM uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Kata ya Mbuguni, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka akitamba mbele ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni za CCM katika mji mdogo wa Mbuguni, jana.
No comments:
Post a Comment