Kiongozi wa Kanisa la Uamisho Mkuu amewataka viongozi wa dini kuwahamasisha Watanzania na viongozi wa serikali kuukaribisha mwaka wa fedha kila unapoanza kwa Dua na Maombi sambamba na suala la bajeti ya taifa ambalo litatoa dira ya Mwelekeo wa uchumi kulingana na vyanzo vya mapato.
Akizungumza jijini Dar es salaam, Kiongozi wa kanisa hilo Mchungaji Naaman Shauri amesema lengo kuu la maono hayo ni kuamsha ari kwa viongozi wote wa dini.
Kanisa la Uamsho Mkuu litakuwa sambamba na serikali katika kuhakikisha kwamba wananchi wote hasusani walioko vijijini wanakuwa na uelewa kuhusiana na Bajeti ya Serikali katika mwaka husika.
No comments:
Post a Comment