Wednesday, October 12, 2011

WANAHARAKATI WAOMBWA KUISHINIKIZA SERIKALI KUTUNGA SHERIA ITAKAYOMTAMBUA MWANAMKE KUWA MMILIKI ARDHI!

Wanaharakati nchini wameombwa kuishinikiza serikali kutunga sheria itakayomtambua mwanamke kuwa ni mmoja ya watu wanaotakiwa kutia saini wakati shamba au ardhi inauzwa na mwanaume ili kuondoa ukiritimba wa mfumo dume unaomdidimiza mwanamke kimaendeleo.

Akizungumza na kituo hiki BI MARTHA TEMBA ambaye ni mkazi wa Moshono mkoani Arusha amesema kutokana na mfumo dume sauti za wanawake kwenye maamuzi ya ardhi hazipewi kipaumbele jambo ambalo halina budi kutiliwa mkazo ili mgawanyo wa ardhi uwe sawa kwa makundi yote.


Baadhi ya vifungu vya sheria ya ardhi vimekuwa vikitoa mamlaka kwa kwa mktano wa kijiji kugawa au kutoa ardhi ekari 50 bila kuingiliwa jambo linalotoa mwanya kwa wawekezaji wasio waaminifu kupora haki ya wanakijiji husika.

No comments:

Post a Comment