Tuesday, July 12, 2011

WABUNGE WAHOJI SERIKALI KUENDELEA KUIBEBA BOHARI YA DAWA NCHINI (MSD)!

Baadhi ya wabunge wamehoji hatua ya Serikali kuendelea kupigania Bohari ya Madawa nchini (MSD), katika manunuzi na usambazaji wa dawa nchini Kufuatia kuwepo kwa malalamiko dhidi ya watendaji wa Idara hiyo

Akichangia bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kwa mwaka 2011 na 2012, Mjini Dodoma Mbunge wa Viti Maalum Kupitia CHADEMA SUSAN LYIMO, amesema watendaji wa Idara hiyo wamekuwa hawazingatii Sheria ya manunuzi ya umma sanjari na manunuzi ya vifaa visivyokidhi viwango


Naye Mbunge wa Viti maalum ( CUF), THUWAYBA MUHAMED, amesema madawa mengi ambayo yamekuwa yakiingizwa nchini wakati muda wake wa kutumika ukiwa umeisha,hali ambayo inaweza kuhatarisha afya na usalama wa wananchi.

No comments:

Post a Comment