Tuesday, July 12, 2011

KANSELA ANGELA MERKEL ATANGAZA KUSAIDIA KUKABILIANA NA UKAME AFRIKA MASHARIKI!

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametangaza kuwa serikali yake itachangia pesa kusaidia juhudi za kukabiliana na ukame Afrika Mashariki.
Bi Merkel amesema Ujerumani itatoa Euro 1 million katika mfuko wa kusaidia walioathirika na njaa katika ukanda wa Afrika Mashariki.


Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya watu milioni 10 wanakabiliwa na njaa kufuatia kipindi kirefu cha ukame na wanahitaji misaada ya dharura.Walioathrika zaidi ni raia wa Somalia, nchi ambayo imekumbwa na vita kwa zaidi ya miaka 20.


Kansela wa Ujerumani ametangaza mchango huo katika mkutano kati yake na Rais Mwai Kibaki mjini Nairobi ambapo ameanza ziara rasmi ya nchi tatu barani Afrika.

No comments:

Post a Comment