Tuesday, July 5, 2011

SHUHUDIA MAZOEZI YA PIKIPIKI KWENYE VIWANJA VYA TANGANYIKA PACKERS KAWE JIJINI DSM!

Mwendesha Pikipiki wa Kambi ya Kinondoni, Ludan Volvo, akionyesha mbwembwe za kutembea na tairi moja wakati wachezaji wa mchezo huo walipokuwa katika mazoezi ya kawaida ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Waendesha Pikipiki, Adil Othman (mbele) akichuana na Ludan Volvo, wakati wa mazoezi yao ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Adil ni mtaalam wa kutumia Pikipiki yenye matairi manne aina ya Quad Bike na Volvo ni mtaalam katika pikipiki ya matairi mawili, hapa wakionyeshana ujuzi.
Waendesha Pikipiki wakianza mwendo kwa pamoja wakati wakishindana katika mazoezi yao ya kujiweka fiti kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mwendesha Pikipiki, Adbul, akiwa hewani baada ya kuruka Tuta, wakati wa mazoezi ya waendesha Pikipiki yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.
Mwendesha Pikipiki, Ludan Volvo, akiwa hewani baada ya kuruka Tuta, wakati wa mazoezi ya waendesha Pikipiki yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam.
Mwendesha Pikipiki, Adil Othuman, akionyesha uwezo wa kuitumia pikipiki ya matairi manee aina ya Quad Bike, wakati wa mazoezi ya waendesha pikipiki hao yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es Salaam. Picha na Sufianimafoto.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment