Tuesday, June 7, 2011
LICHA YA KUTUMIA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 798 SERIKALI YASHINDWA KUMALIZA TATIZO LA MGAO WA UMEME!
Serikali imesema licha ya kuwekeza takribani Dola za Kimarekani milioni 798 kwenye sekta ya umeme tangu kipindi cha uongozi wa awamu ya pili mpaka sasa imeshindwa kumaliza kabisa mgao wa umeme kutokana na mahitaji makubwa ya nishati hiyo yanayochangiwa na kukua kwa uchumi.
Akijibu swali la nyongeza kwenye Bunge la kumi, mkutano wa nne, Bunge la Bajeti kikao cha kwanza, Naibu Waziri wa Nishati na Madini ADAM MALIMA amesema hata kama mitambo yote inayozalisha umeme itafanya kazi mgao wa umeme hautakwisha kwani kuna upungufu wa Megawati 260 unaotokana na ongezeko la matumizi ya umeme kwa asilimia 13 kila mwaka.
Katika swali lake la nyongeza Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Bunda, ESTHER BULAYA alimuuliza Naibu Waziri MALIMA kuwa licha ya serikali kuorodhesha miradi mipya ya umeme, ni lini itatoa tamko kuhusu kukoma kabisa kwa mgao wa umeme.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment