Friday, July 1, 2011

DK MAUA DAFTARI AHOJI UHALALI WA DAWA YA MCHUNGAJI MWASAPILA!

Mbunge wa Viti Maalum Dk.MAUA DAFTARI (CCM) ameihoji Serikali kama katika utafiti wake uliofanywa na Wizara ya Afya kuhusiana na dawa ya Mchungaji Ambilikile Mwasapila kama wamebaini inatibu magonjwa sugu ukiwemo ugonjwa wa kisukari.

Hata hivyo Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. LUCY NKYA amesema kuwa tayari wameiagiza taasisi ya magonjwa ya Binadamu NIMR kuchunguza kama dawa hiyo inatibu magonjwa sugu.
Amesema utafiti huo tayari umeshaanza na matokeo ya uchunguzi huo yatatolewa baada ya zoezi la utafiti huo kukamilika.

No comments:

Post a Comment