Friday, July 1, 2011

WAFUGAJI WATAKIWA KUELIMISHWA MADHARA YA KUWEKA ALAMA KWENYE MIFUGO!

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, imeshauriwa kutoa elimu kwa wafugaji kufuatia walio wengi kuwa na utamaduni wa kuweka alama kwenye ng’ombe zao na haki inayosababisha baadhi ya ngozi zizanazozalishwa kukosa ubora.

Akizungumza katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mareshi shoe maker, PRISCUS MARESHI, amesema sehemu zenye chapa husababisha kupungua kwa thamani ya ngozi hizo na kwamba Watanzania wameanza kuhamasika na bidhaa zinazozalishwa nchini.
Katika hatua nyingine, Bwana MARESHI, amesema kwa sasa bidhaa zinazozalishwa nchini zimeanza kuwa na soko hali inayosaidia kuongeza ushindani dhidi ya bidhaa kutoka nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment