Monday, July 11, 2011

DK BILAL AFUNGUA KIGODA CHA MWALIMU KINACHOSIMAMIA MAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI!

                         Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kilichozinduliwa leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kumbukumbu ya Kigoda cha Mwalimu Nyerere kinachohusika na masuala ya Mazingira na mabadiliko ya Tabianchi, kilichozinduliwa leo Julai 11, 2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutangazwa kwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda hicho, Prof. Pius Yanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Prof. Pius Yanda, baada ya kutangazwa na kuvishwa Joho la kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kigoda hicho uliofanyika leo Julai 11, 2011 katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Pius Yanda, akiwa ameketi kwenye Kigoda hicho baada ya kutangazwa rasmi wakati wa uzinduzi huo. Picha na Muhidin Sufiani.

No comments:

Post a Comment