Monday, July 11, 2011

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA MFUKO WA KUCHANGIA MADAWATI WA HASSAN MAAJAR TRUST!

Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mume wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bwana MAAJAR.

Watanzania wametakiwa kutambua kwamba serikali ni wananchi na sio viongozi na hivyo wanatakiwa kuchangia masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kutatua suala la upungufu wa madawati milioni tatu unaozikabili shule za msingi na sekondari nchini.

                     Balozi Maajar akizungumza kabla ya kumkaribisha Mama Salma Kikwete.

Akizindua Mfuko wa Kuchangisha Madawati wa Hassan Maahar TRUST Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Tanzania WAMA, Mama SALMA KIKWETE amesema kwamba wananchi wengi wamekuwa ni watu wa kulaumu badala ya kuwa mstari wa mbele katika kuchangia masuala ya kijamii.
                Mama Salma Kikwete akionesha nembo ya mfuko huo kuashiria uzinduzi rasmi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Kuchangisha Madawati wa Hassan Maahar TRUST, Balozi wa Tanzania nchini Marekani MWANAIDI MAAJAR ametoa wito kwa Watanzania waliosomeshwa na serikali kurudisha kwa jamii angalau kile kidogo walichonacho kwa kuchangia ununuzi wa madawati.
Wadau mbalimbali walikuwepo kuunga mkono uwepo wa mfuko huo utakaochangia madawati nchini.
Wanafunzi ambao ni waathirika wahanga wa madawati shuleni walikuwepo kuwakilisha.

Wakati wa uzinduzi huo jumla ya shilingi Milioni tisa nukta tano zilichangwa na wadau mbalimbali ili kukabiliana na upungufu wa madawati milioni 3 unaolikabili taifa kwa sasa.

No comments:

Post a Comment