Friday, July 1, 2011

WABUNGE WAITAKA SERIKALI KUFUATILIA CHANZO CHA MIGOMO VYUONI!

Baadhi ya Wabunge wameitaka Serikali kuchunguza kwa kina kuhusu migomo ya mara kwa mara katika chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na kusababisha chuo hicho kichanga kuonekana ni kinara wa migomo hiyo nchini.

Wamesema kuwa Serikali inatakiwa kuchunguza kwa kina ili kukomesha migomo hiyo katika vyuop mbalimbali nchini hususan Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kimeonekana kuwa kinara wa migomo hiyo.
Pia wamewataka baadhi ya wanasiasa kuacha tabia ya kueneza siasa katika chuo hicho kufuatia kusadikika kuwa huchangia migomo ambayo haina tija kwa wanafunzi na Taifa kwa ujumla.
Wabunge hao wameyasema hayo wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya waziri Mkuu kwa mwaka 2011/2012 mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment