Sunday, June 26, 2011

WALANGUZI UFUTA KILWA KUKIONA:NAPE

                                   Wakulima wakiangalia moja ya Sahamba la Mpunga

NA BASHIR NKOROMO, LINDI
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,ametangaza kiama cha walanguzi wa ufuta kwa kuitaka serikali ya wilaya ya kilwa na mkoa wa Lindi kuhakikisha inakomesha ulanguzi huo mara moja.


Nape alitoa agizo hilo kwa nyakati tofauti katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika mji mdogo wa Kilwa Kivinje na Kilwa Masoko katika ziara ya siku mbili ya baadhi ya wajumbe wa Sekretariti ya CCM mkoani Lindi katika kufikisha ujumbe wa maamuzi ya NEC yaliyofanyika mjini Dodoma Aprili mwaka huu.

Nape alisema kinachoendelea kwa walanguzi wanaokwepa mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye ununuzi wa ufuta ni hujuma kwa wakulima na serikali ya CCM kama mtetezi wa wanyonyonge hasa wakulima haiwezi kukaa kimya na kuangalia wakulima wakidhulumiwa haki zao.


Kwa mujibu wa Nape wapo viongozi wa kisiasa wanaongoza dhuluma hiyo kwa kisingizio cha kuwasaidia wakulima wakati ukweli wanawadhulumu na kumshushia tuhuma hizo mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Bungala ‘Bwege’ kuwa ndio kinara dhuluma hiyo.


“Naambiwa mbunge wenu bwana ‘Bwege’ kaacha bunge la bajeti na kuja kusimamia dhuluma yake dhidi ya wakulima masikini wa ufuta. Bwege rudi bungeni kama hujui kazi yako ni kuwatetea wananchi basi bora ujiuzulu wananchi wapate mwakilishi na si mlanguzi” alisema Nape.

No comments:

Post a Comment