Tuesday, May 10, 2011

SHAMSI VUAI NAHODHA ALAANI KITENDO CHA UCHOMAJI MABANDA UNGUJA!

                                                         SHAMSI VUAI NAHODHA

Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi SHAMSI VUAI NAHODHA, amelaani vikali kitendo cha Uchomaji wa vibanda 73 vya Biashara kilichofanywa Mjini Unguja ambapo zaidi ya watu 7 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi kufuatia tukio hilo.

Akizunguza na Waandishi wa Habari, Mjiji Dodoma kuhusiana na tukio hilo Waziri NAHODHA amesema tukio hilo hawezi kulihusisha na masuala ya kisiasa wala muungano.

Amesema tukio hilo la Uchomaji wa Vibanda hivyo ni chuki Binafsi miongoni mwa Watu wachache wasiopenda maendeleo ya watu wengine,ambapo sanjari na hatua hiyo ametaka vyombo vya Dola Viachwe vifanye kazi yake ili kubaini undani halisi wa Tukio hilo.

Aidha Bwana Shamsi Vuai amesema kitendo hicho kimelenga moja kwa moja katika suala la Uvunjifu wa Amani na uvunjaji wa Sheria za Nchi,ambapo amewataka wananchi kuwa watulivu wakati vyombo vya Dola vikiendelea na kazi yake ya Uchunguzi ili watakaobainika waweze kufunguliwa mashtaka kutokana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment