Sunday, July 24, 2011

NAPE AKAMATA NYARAKA ZA UCHOCHEZI ZINAZODAIWA KUSAMBWA NA CHADEMA!

NA MWANDISHI WETU, MOSHI

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amedai kuzinasa nyaraka za zinazosambazwa na CHADEMA nchi nzima kuchochea maandamano na kuzuia wananchi kuchangia shughuli za maendeleo nchi nzima.

Akizungunza katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye Stendi Kuu ya mabasi mjini Moshi, Nape alisema, nyaraka alizonasa ni pamoja na baruza yenye kumbukumbu namba CDM/DSM/HU/Vol 040/2011 ya Julai 20, 2011, ambayo CHADEMA imewasambazia wenyeviti wa chama hicho kila mkoa kuchoandaa maandamano nchi nzima baada ya kikao cha Bunge la bajeti.


Kwa mujibu wa Nape barua hiyo ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CAHDEMA, Erasto Tumbo barua hiyo inashinikiza wenyeviti hao kutekeleza maamuzi ya Kamati Kuu ya chama hicho kuandaa maandamano hayo ili kuiwaibisha serikali kwa madai kwamba imeshindwa kutekeleza majukumu ya kuwaletea maendeleo wananchi.


“Ni jukumu lako Mwenyekiti na makatibu wa majimbo katika mikoa kuanza kuhamasisha wananchi na kupanga wafuasi kikamilifu kwani harakati za awamu hii ni ndefu sana baada ya vikao vya bunge”, Nape alinukuu sehemu ya barua hiyo ambayo aliionyesha katika mkutano huu.


Alisema barua nyingine ni yenye kumbukumbu namba CDM/DSM/ Vol. 138/2011 ya Juni 30,2011 ambayo pia imesainiwa na Tumbo iliyosambazwa kwa Makatibu wa Majimbo kutakiwa kutekeleza agizo la Kaatibu Mkuu wa CHADEMA Wilborod Slaa kuhamasisha wananchi wagome shughuli za maendeleo.


Barua hiyo ambayo Nape aliionyesha mkutanoni ina kichwa ‘ Utekelezaji wa agizo la Katibu Mkuu kuhamasisha wananchi wagome kuchangia shughuli za maendeleo”.

No comments:

Post a Comment