Wizara ya Ujenzi imewasilisha Bajeti yake ya Mwaka 2011/2012 Bungeni mjini Dodoma na kusema katika mwaka huu wa fedha wizara hiyo inakadiria kukusanya mapato ya shilingi Trilioni 1.4/- ambapo shilingi Bilioni 15.8 zitatumika kwa ajili ya mishahara ya wafanyakazi, mfuko wa barabara umetengewa shilingi Bilioni 221.5 na matumizi mengine yatagharimu bilioni 7.9.
Akisoma bajeti hiyo Bungeni mjini Dodoma Waziri wa Ujenzi DK JOHN MAGUFULI amewaomba wabunge wote bila kujali itikadi za kisiasa kupitisha makadirio ya wizara hiyo na kubainisha kuwa kujenga barabara ni kuinua uchumi.
No comments:
Post a Comment