Monday, July 18, 2011

SERIKALI YATAKIWA KUTOA HISA KWA VIJIJI VYA MIGODINI!

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeshauriwa kutoa hisa ya asilimia tatu kwa vijiji vinavyozungukwa na migodi ya madini ili wananchi wa maeneo hayo waweze kunufaika na rasilimali zilizopo katika maeneo yao ikiwemo kujengwa kwa vituo vya afya na shule za kisasa.

Akichangia hoja ya Wizara ya Nishati na Madini Bungeni mjini Dodoma Mbunge wa Viti Maalum (CCM) ESTHER BULAYA ameshangazwa na kitendo cha serikali kushikwa na kigugumizi katika kutoa maamuzi kwa wawekezaji wanaochimba madini nchini na kuwanyonya Watanzania hali inayosababisha migogoro baina ya wawekezaji na wananchi.


Kwa upande wa ukosefu wa umeme alisema vijana ambao ni asilimia 60 ya Watanzania miongoni mwao hususani wale waliojiajiri wanashindwa kufanya kazi zao ipasavyo baada ya kukosa nishati hiyo muhimu katika kufanikisha kazi zao.

No comments:

Post a Comment