Mamlaka ya Majisafi na Majitaka mjini Dodoma(DUWASA) imesema hali ya kuziba kwa mitandao ya majitaka mara kwa mara inatokana na vitendo vya wananchi katika manispaa hiyo kutupa taka ngumu katika mitandao hiyo.
Akizungumza na Kituo hiki mkoani Dodoma Afisa uhusiano wa mamlaka hiyo Sebastian Warioba amesema hali hiyo imekuwa ikiisababishia hasara kubwa Duwasa kutokana mitandao hiyo kuhitajika kuzibuliwa mara kwa mara kwa lengo la kuweka mazingira safi ili kuepuka magonjwa ya milipuko.
Kufuatia hali hiyo Afisa Uhusiano huyo amewataka wananchi wa mji wa Dodoma kuitumia mitandao hiyo vizuri na siyo kutupa taka ngumu zinazoweza kusababisha kuziba kwa mitandao hiyo.
No comments:
Post a Comment