Wednesday, November 2, 2011

SERIKALI YAUTAKA MFUKO WA HIFADHI LAPF KUWAELIMISHA WANACHAMA WAKE UMUHIMU WA KUCHANGIA KWENYE MFUKO HUO!

Serikali imeutaka mfuko wa jamii LAPF kuwaelimisha wanachama wake umuhimu wa kuchangia michango kwa wakati ili Mfuko huo uweze kuwahudumia kwa ufanisi na kwa haraka zaidi.

Akifungua mkutano wa nne wa wadau wa LAPF unaofanyika jijini Dar es Salaam Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema kwamba inasikitisha kuona baadhi ya waajiri hawawasilishi michango kwenye mfuko huo licha ya mishahara yao kukatwa.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Kept GEORGE MKUCHIKA amewaagiza Makatibu Tawala kote nchini kuwachukulia hatua za kisheria watendaji wa serikali watakaoshindwa kuwasilisha kwa wakati michango ya wafanyakazi kwenye Mfuko wa Penseni wa Serikali za Mitaa LAPF.
Akizungumza kwenye Mkutano wa nne wa LAPF unaofanyika jijini Dar es Salaam Waziri MKUCHIKA amesema kuwa hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi ni moja kati ya haki za msingi za mtumishi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw ELLIUD SANGA amesema mfuko huo umeongeza kiwango cha makusanyo kutoka shilingi Bilioni 54.2 mwaka 2009/2010 hadi kufikia Bilioni 75.5 mwaka 2011.
                                             Kepteni Mstaafu GEORGE MKUCHIKA.

No comments:

Post a Comment